Ronaldo set to come back to man united
Mchezaji bora wa dunia raia wa Ureno na klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemtaka wakala wake mashuhuri, Jorge Mendes afanye kila lililo juu ya uwezo wake kuhakikisha anarejea Manchester United.
Cristiano Ronaldo ana muhimiza Meneja wake ahakikishe anarejea Manchester United
Manchester wako tayar kutoa €175 pamoja na Degea ili kumnasa mchezaji huyo
Manchester wako tayar kutoa €175 pamoja na Degea ili kumnasa mchezaji huyo
Nyota huyo wa Real Madrid ameyasema hayo siku ya Ijumaa ikiwa ni mara baada ya kuingia katika shutuma za ukwepaji wa kodi inayofikia paundi milioni 13 hali iliyosababisha kumuambia wakala wake Mendes ahakikishe anafanya kila liwezekanalo ndoto za kurudi United zinatimia.
Mpaka sasa klabu ya United, Chelsea, Paris Saint-Germain pamoja na Bayern Munich zimeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya mreno huyo ambaye kwa sasa yupo na timu yake ya taifa katika michuano ya mabara inayoendelea huko nchini Urusi.
Man Utd, Chelsea, PSG pamoja na Bayern Munich zimeonesha nia ya kuhitaji huduma Ronaldo mwenye miaka 32
Matajiri wa Ufaransa PSG imetenga kitita cha paundi milioni 122m kwaajili ya uhamisho wake huku wakitarajia kumlipa mshahara wa paundi 26m kwa mwaka.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anadhani bado kuna kazi hajaimaliza Old Trafford lakini pia haitaji kuikosa nafasi ya kurejea kama shujaa ndani ya klabu yake ya zamani ya United.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anadhani bado kuna kazi hajaimaliza Old Trafford lakini pia haitaji kuikosa nafasi ya kurejea kama shujaa ndani ya klabu yake ya zamani ya United.
No comments