Weusi kudondosha video mbili "yakulevya" na "dude"
Kundi la hip hop Bongo, Weusi limeweka wazi kuwa video ya wimbo ‘Yakulevya’ itatoka pamoja na video ya wimbo ‘Dude’ uliotoka jana.
Rapper Nikki wa Pili amesema kuwa maandalizi yote tayari ila bado vitu kitu vichache lakini baada ya wiki moja watadondosha video zote kwa pamoja.
“Ni zote Dude na Madaraka ya Kulevya kwa sababu Yakulevya ni deni kubwa. Hatuja tenda haki kuichelewesha kutoa, deni letu kubwa ni kwamba itabidi tufanye video kubwa ili kulipa deni,” Nikki amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM
Kwa upande wake Joh Makini amesema Madaraka ya Kulevya na mazingira yake jinsi ilivyotengenezwa ni kama Dude, hivyo wimbo kama huo ukiuacha uje utoe kama miezi sita ijayo hautaleta maana.
“Ingawa wimbo mkali haupitwi na wakati siku zote, kwa hiyo tumeona huu wimbo ni wa moto na ndio wakati wake tukasema tukisubiri video tunaweza tukachelewa na muda ndio ule ule na hatuwezi kulipua kushoot video ya kawaida kwa sababu ya kutoa tu wimbo na video,” ameleeza Joh Makini.
No comments